Jumamosi 15 Novemba 2025 - 22:34
Tumejikita katika silaha za muqawama na Wito Wowote wa Kujisalimisha ni Usaliti kwa Damu za Mashahidi

Hawza/ Jumuiya ya Maulama wa Kiislamu wa Lebanon katika tamko lao wamesema kuwa; mwaka huu umechukua sura ya kipekee, kwa sababu msafara wa mashahidi umeungana na Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin pamoja na idadi kubwa ya makamanda.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Maulama wa Kiislamu wa Lebanon katika tamko lao wametaja kuwa mwaka; huu umechukua sura ya kipekee, kwa sababu msafara wa mashahidi umeungana na shahidi mtukufu na mtakatifu wa umma, Sayyid Hassan Nasrallah (quddisa sirruh), na Sayyid Hashim Safiuddin (ridhwanullahi alayh), pamoja na idadi kubwa ya makamanda wa ngazi za juu wa muqawama na mamia ya mujahidina waliouawa kishahidi.

Jumuiya hiyo ikaongeza: Tunapowakumbuka mashahidi hawa na watangulizi wao katika njia hii yenye nuru, tunasisitiza juu ya kuendeleza na kuthibitisha njia hii. Shada haipunguzi safu za mujahidina, bali ni sababu ya kuongezeka kwao, kukua kwao na kuimarika kwao katika kushikamana na njia ya mashahidi. Kwa sababu hiyo, kauli mbiu ya mwaka huu imetokana na maneno matukufu ya shahidi mtukufu Sayyid Hassan Nasrallah (quddisa sirruh) aliposema: “Wakati tunapouawa kishahidi, tunashinda.”

Jumuiya ya Maulama ikaeleza kwamba: Hii ni kwa sababu kuwa; shahada inatimiza ushindi binafsi — kupitia kufikia lengo tukufu la maisha ambalo ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuungana na msafara wa mashahidi wenye nuru — na pia inaleta ushindi kwa umma, kwa kuwa tumesimama hadi mwisho na hatukuiruhusu adui Mzayuni kutimiza malengo ya uvamizi wake. Zaidi ya hapo, kwa matendo yetu tumeonesha kuwa tumejikita katika mstari wa muqawama na tuko tayari kutoa roho zetu katika njia hii.

Tamko hilo likaendelea: Leo tunapoona wingi huu mkubwa wa watu wakijikusanya kuzunguka muqawama — katika mazishi ya mamilioni ya watu ya mashahidi wawili wakubwa, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim (ra) — na tuliposhuhudia mkusanyiko mkubwa katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kuuawa shahidi wao, na pia tulichokiona katika mkusanyiko mkubwa zaidi katika historia ya Harakati ya “Vinara wa Imam Mahdi (aj)” katika uwanja wa michezo, tunasisitiza kuwa shahada haijasababisha kurudi nyuma wala udhaifu, bali imeleta ukuaji wa uelewa kwa umma na kuongezeka kwa uthabiti wake katika njia ya muqawama. Kama alivyosema Imam Khomeini (quddisa sirruh): “Tukiuliwa, taifa letu linakuwa macho zaidi.”

Jumuiya ya maulama ikabainisha kwama: Sasa tunasisitiza kuwa zaidi ya hapo tumejikita katika silaha na njia yetu, hatutakabidhi silaha, na tutaendelea kubaki kwenye uwanja hadi tuupate ushindi wa mwisho dhidi ya adui Mzayuni. Na katika tukio hili kubwa, tunasisitiza mambo yafuatayo:

Mosi: Hatukubali wito wowote wa kusalimisha silaha za muqawama, na tunauona kuwa ni usaliti kwa damu ya mashahidi. Tunasema wazi kuwa tutazilinda silaha hizi hadi ushindi wa mwisho dhidi ya adui Mzayuni utakapopatikana.

Pili: Tunasistiza juu ya kushikamana na azimio namba 1701 la makubaliano ya kusitisha mapigano; tumetekeleza wajibu wetu katika makubaliano haya, na ni adui Mzayuni anayepaswa kutekeleza sehemu yake — ikiwemo kuondoka katika ardhi yote ya Lebanon iliyo chini ya uvamizi, kuwaachia huru wafungwa wote, na kusimamisha uvamizi wa kila siku ardhinj, baharinj na angani.

Tatu: Hakuna mjadala wowote unaokubalika kuhusu suala la “kunyang’anya silaha” ila tu baada ya adui Mzayuni kutekeleza kikamilifu ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano na azimio 1701, na baada ya kukamilika upya wa ujenzi wa uharibifu wote uliosababishwa na vita.

Nne: Hatuihesabu Marekani kuwa ni mpatanishi katika mgogoro kati ya Lebanon na adui Mzayuni; bali ni mshirika katika mgogoro huu, anayemuunga mkono na kumsimamia adui Mzayuni, na kwa msingi huu lazima ashughulikiwe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha